Lang: SW | EN
🔄

Zungusha na Geuza Mwelekeo wa Picha Yako Hapo Hapo

Umescan au kupiga picha ikakaa pembeni au kichwa chini? Rekebisha mwelekeo wa picha za JPG, PNG na WEBP kwa urahisi. Mfumo ni salama 100% kwani picha haipakiwi kwenye server yoyote.

Kwa Nini Mwelekeo wa Picha Ni Muhimu?

Unapopakia picha au nyaraka kwenye mifumo ya maombi ya kazi (kama Ajira Portal, UTUMISHI, NIDA, au Vyuo), mifumo hiyo ya kiotomatiki inasoma vyeti au picha kuanzia juu kwenda chini. Kama picha imepinda au ipo kando, afisa anayekagua anaweza kuiruka au mfumo ukakataa QR Code. Zana hii ya GridPhoto inakusaidia kuweka picha katika uelekeo sahihi kwa sekunde chache.

🔒 Utunzaji wa Faragha (Client-Side HTML5 Processing) Picha yako haijumbe au kuhifadhiwa kwenye server zetu za nje. Zana yetu inatumia teknolojia ya HTML5 Canvas kugeuza picha moja kwa moja ndani ya kivinjari cha simu au kompyuta yako.

Zana Hii Inatunzwa na Kuendeshwa na Kizumari Technologies | Mhandisi Suleiman Nassoro Ally

Maswali Yanayoulizwa Sana (FAQ)

❓ Je, nikizungusha au kugeuza picha ubora wake utapungua? Hapana kabisa! Mfumo wetu unahifadhi ubora, rangi, na uwazi halisi wa picha yako bila kuisawazisha kwa kiwango kinachoharibu muonekano.
❓ Je, ni salama kurekebisha vyeti na nyaraka zangu hapa? Ndiyo, ni salama 100%. Mchakato wote unafanyika ndani ya kivinjari (browser) cha kifaa chako, hivyo hakuna mtu mwingine anayeweza kuona au kuipakua picha yako.
❓ Tofauti kati ya Flip Horizontal na Flip Vertical ni ipi? Flip Horizontal inageuza picha kama vile inaangalia kwenye kioo (kushoto kwenda kulia), wakati Flip Vertical inageuza picha kutoka juu kwenda chini.